Vi bøger
Levering: 1 - 2 hverdage
Forlænget returret til d. 31. januar 2025

Bøger udgivet af Mkuki na Nyota Publishers

Filter
Filter
Sorter efterSorter Populære
  • af Marc Eichen
    248,95 kr.

    "The stories in Wind, Sand, Sky are short, but rich with meaning. Set on the East African archipelago of Zanzibar, these intimate portraits invite the reader to accompany characters navigating personal challenges within a rapidly changing terrain linked to socio-economic development, tourism, and even climate change. The book will be of interest to students of Swahili and East Africa, and more broadly those seeking to understand the cultural tensions and transformations associated with globalization.- Caitlyn Bolton, PhD Assistant Professor, Boston College"Wind, Sand, Sky by Marc Eichen is an incredibly thoughtful, unique and special bilingual English- Swahili work of art that both English and Swahili audiences will not only find thrilling, but also superbly depicting some segments of the Swahili-speaking society and cross-cultural engaging - a bonus for Kiswahili students as a sample source that intrinsically integrates the World-Readiness Standards for Learning Languages five goal areas (5 Cs): Communication, Cultures, Connections, Comparisons, and Communities.- Charles Bwenge, PhDInstructional Professor of African Languages, University of Florida

  • af Peter Singer
    483,95 kr.

    "If I have to choose the book that brought me a big change, then I would say Animal Liberation by Peter Singers." -Jane Goodall"Singer's documentation is unrhetorical and unemotional, his arguments tight and formidable, for he bases his case on neither personal nor religious nor highly abstract philosophical principles, but on moral positions most of us already accept." -New York Times Book Review"A most important book that will change the way many of us look at animals-and, ultimately, at ourselves." -Chicago Tribune"This book is a must . . . not just for every animal lover but for every civilized reader." -Cleveland Amory"Kama nisingekuwa na budi kuchagua kitabu kilichoniletea mabadiliko makubwa, basi ningesema 'Ukombozi wa Wanyama' cha Peter Singer." - Jane Goodall"Muundo wa uwasilishaji ujumbe wa Singer si wa kimazoea na haufungwi na hisia; ujengaji wake wa hoja ni makini na wenye fikra nzito, kwani hajengi hoja zake kwenye kanuni binafsi wala zakidini wala falsafa ya hali ya juu ya kufikirika, bali katika misimamo ya kimaadili ambayo wengi wetu tayari tunaikubali." - New York Times Book Review"Ni kitabu muhimu sana ambacho kitabadili namna wengi wetu tunav-yowachukulia wanyama-na, hatimaye, sisi wenyewe." - Chicago Tribune"Kitabu hiki ni cha lazima...si kwa wapenda wanyama tu bali kwa kila msomaii alivestaarabika." - Cleveland AmoryTangu chapisho la kwanza kabisa la mwaka 1975, kazi hi yenye kuleta mageuzi makubwa imewaamsha mamilioni ya watu katika kung'amua uwepo wa "uspishi"-kutokuiali kwetu kwa kimfumo dhidi va wanvama wasio binadamu-na hivyo kuchochea harakati kote ulimwenguni za kuleta mabadiliko katika mitazamo yetu kuhusu wanyama na kukomesha kabisa ukatili tunaowatendea.Katika Ukombozi wa Wanyama, mwandishi Peter Singer anaanika uhalisia wa kutisha wa "mashamba-viwanda va kisasa" tulivonayo na hatua za upimaji bidhaa-akitungua hoja muflisi za utetezi, na kupende-keza mbadala wa kile ambacho kimekuja kuwa suala zito la kimazingira na kiiamii na vilevile la kimaadili. Huu ni wito muhimu na unaofikirisha kwa dhamiri, usawa, ustaarabu, na haki na ni andiko la msingi lenye kusha-wishi kwa waunga mkono na hata kwa watia shaka.

  • af Marc Eichen
    298,95 kr.

    Katika miaka zaidi ya 20 ya kufundisha Kiswahili kwa wageni, sija-kutana na andiko la hadithi nzuri kama hizi alizoandika mwandi-ihi Marc Eichen. Ufundi wake wa kutumia vitushi halisi, na kuvis-ana kwa maumbo mbalimbali ya lugha ni wa kipekee! Hadithi tatu hizi ni mchango mkubwa katika ufundishaji wa Kiswahili na fasihi kwa wenyeji na ugenini. Zitawasaidia pakubwa walimu pamoja na wanafunzi kufahamu uhondo wa lugha za Kiswahili na Kiingereza kupitia vipengele mbalimbali vya lugha aliyotumia mwandishi. Ndugu Suleiman Khalfan na Abdulrahman Ndegwa vilevile wametoa tafsiri ya haki, wakilenga kabisa alichodhamiria mwandishi wa hadithi zenyewe.- Dr. David KyeuCoordinator and Continuing LecturerCenter for African StudiesUniversity of California, BerkeleyHadithi katika kitabu cha Upepo, Mchanga, Anga ni fupi, lakini zenye maana. Hadithi hizi zimejikita katika mandhari ya visiwa vya Zanzibar, Afrika Mashariki, taswira hizi za wazi zinamwalika msomaji kuandamana na wahusika wanaopitia changamoto za kibinafsi ndani ya eneo linalobadilika kwa kasi kutokana na maendeleo ya kijamii na kiuchumi, utalii, na hata mabadiliko ya tabianchi. Kitabu hiki kita-wavutia wanafunzi wa Kiswahili na Afrika Mashariki kwa ujumla, na kwa upana zaidi, wale wanaotaka kuelewa mivutano ya kitamaduni na mabadiliko yanayohusiana na utandawazi.- Caitlyn Bolton, PhD Chuo cha Boston

  • af Sylvester Barongo
    332,95 kr.

    Meet the Founder of Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) as he takes you on a journey through his career in the oil and gas sector, and how important events and wars in the industry impacted Tanzania in the 1970s. He describes the actual events on the field, the challenges faced from the founding of TPDC to the beginning of exploration in Tanzania, the global trans- formation of oil and gas in real time, how it was dealt with, and how the Tanzanian economy has benefited greatly from the gas discovered during his tenure. Mr. Barongo presents an honest account of why various actions were made despite the fact that the outcome was unpredictable. The government trusted him and his strong team because of their faith, confidence, and belief, and they were left alone to make the vital decisions that led to Tanzania's oil and gas boom. Since then, Tanzania has attracted a slew of investors looking to engage in oil and gas, including the current Liquefied Natural Gas (LNG) project, which is valued at $30 billion.

  • af Halfani Sudy
    651,95 kr.

    Askari wa kike, Hannan Halfani anagundua siri kubwa ya kupangwa kwa mpango wa kumuua rais Mark Mwazilindi akiwa katika maliwato ya ikulu. Kutoka katika mdomo wa Hannan, anaisafirisha siri hiyo hadi katika sikio la mpelelezi mahiri nchini Tanzania, Daniel Mwaseba. Daniel na Hanna wakishirikiana na mpelelezi wa kujitegemea, Martin Hisia, wanaingia kazini na kuanza kuchunguza kisa cha kupangwa kwa kifo cha rais. Unakuwa ni uchung uzi mgumu sana. Uchunguzi unaowa-pitisha katika msitu mnene na unaowapitisha katika matukio ya kutisha isivyo kawaida. Uchunguzi unaowafanya wawe karibu na kifo kuliko wakati wowote katika maisha yao ya kipelelezi. Kwa hakika, kunakuwa na mstari mwembamba sana kati ya maisha yao na kifo Bila kujua, kumbe walikuwa wameingia katika anga hatari sana za wafanyabiashara wakubwa wa madawa ya kulevya nchini Tanzania. Madawa ambayo kwa sasa yamekuwa ni KIRUSI KIPYA. Wafanyabiashara hawa wanapanga kumuua rais Mark kwa kuwa amekuwa ni kikwazo kikubwa sana katika biashara zao. Wakina Daniel wanajikuta na kazi kuu mbili ngumu sana kuliko zote walizowahi kuzifanya, ya kwanza ni kuzuia kuawa kwa rais, ya pili ni kuwatia mbaroni watanvabiashara wote wa madawa havo haramu. Je wakina mpelelezi Daniel Mwaseba na wenzake watafanikiwa?

  • af Mohamed Omar Juma
    293,95 kr.

    Jangwa lenye jua kali, Navyo vivuli vichache, Vya miti isiyo hali, Jua linatoa cheche, Safari yenye machofu, Pepo kurusha mavumbi, Wengine wamepofuka. Tumshukuru jalali, Ameiotesha miche, ya miti yenye vivuli, Vya wengi sio wachache, Kiu ilipo- tukifu, Hapo ikabubujika, Chemchemi jangwani. Ni chemchemi jangwani, Yenye maji ya kutosha, Mwenye kiu kukatisha, Mwenye uchafu akoge, Ama ajitoharishe, Majumba yapigwe deki, Nafsi zisuuzike. Maji yaliyosafika, Yenye asili rutuba, Twapata matumaini, Miti yote itashiba, Bustani kupendeza, Na mifugo kunawiri, Videge kuchezacheza, Wala haizuiliki, Mola aipe kibali, Jangwani itamalaki, Walimwengu iwafae, Wagonjwa iwatibie, Joto nalo lififishwe, Kwa Chemchemi jangwani.

  • af Rashid Ali Othman
    333,95 kr.

    Mji wa Kambare ni diwani iliyotungwa kwa umahiri na ustadi wa aina yake kuweza kumvutia kila anayeisoma, awe ni mwanafasihi na mwanaisimu ama mtu wa fani yoyote ile. Hii inatokana na uteuzi mzuri wa misamiati inayolandana vina na mizani kiasi ya kuukonga moyo wa msomaji. Muwala, ufundi mkubwa katika kupangilia maneno, ujenzi wa taswira na lugha ya picha, ubobezi katika kumfikirisha msomaji, upana wa dhamira na maudhui yapatikanayo katika tungo zilizomo ndani ya diwani hii zinagusia takriban nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Kwa kiasi kikubwa, diwani hii imetumia lahaja za kizanzibari, hasahasa kipemba. Pia kuna maneno ya Kiswahili asilia ambayo yametumika kuongeza vionjo vya lugha na utamu wa michapo ya mashairi na tungo za Kiswahili cha uswahilini. Hata hivyo, maneno magumu yamefafanuliwa maana mwishoni ili kukidhi haja ya msomaji wa diwani hii. Kwa ujumla, diwani hii itawafaa sana wapenzi wa lugha ya Kiswahili hususani wapenzi wa mashairi, walumbi wa lugha, wanataaluma, wanafunzi wa ngazi tofauti za elimu, walimu shuleni, wakufunzi vyuoni, wafanyakazi maofisini na taasisi mbalimbali za kielimu, asasi za kijamii, vikundi vya tamaduni na sanaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na vikundi vya ngoma za burudani. Hapana shaka, maendeleo ya lugha na Ushairi wa Kiswahili pamoja na ukuaji wake unaonekana waziwazi endapo utajisomea diwani hii.

  • af Ahmed Hussein Ahmed
    293,95 kr.

    Diwani hii imeandikwa kwa lahaja ya Kimvita, lahaja izungumzwayo jijini Mombasa. Lahaja hii imetumiwa na washairi maarufu pamoja na wazoefu wa tungo katika nyakati mbalimbali kihistoria kama vile Shaha Muyaka wa Muhaji, Ahmad Nassir Juma Bhalo, Abdilatif Abdalla na sasa Ahmed Hussein Ahmed. Hii ni lahaja yenye manyumbulifu anuwai kwa namna sauti zake zinavyoleta maana tafauti zinapotamkwa na ina ukwasi wa misamiati. Mashairi yaliyomo kwenye diwani hii yanaangazia mada mbalimbali zikiwemo, utamaduni wa mwandishi, masuala ya maisha, mijadala ya kielimu, maswali na majibu, taanasi and masuala ya kisasa. Vile vile mshairi ametumia mbinu mbalimbali za tasnifu ya tungo kwa mfano, tathlitha, tarbia na majibizano kufikisha ujumbe wake.

  • af Mbwana Kidato
    373,95 kr.

    Hii ni Riwaya ya kwanza ya Mbwana Kidato ambayo inatokana na tukio la kweli alilolisoma alipokuwa akipitia majarida mbali mbali ya Tanzania kwenye mtandao. Kwenye kurasa za mbele, alikutana na habari ya kuhuzunisha. Ilikuwa ni habari ya msichana mwenye ulemavu wa ngozi aliyekatwa viungo vya mwili wake. Hii ni kazi ya mwandishi, kazi ya kufikirika, yenye kuelimisha, kuakisi maisha yetu na kutuuliza maswali juu ya utu wetu. Je miongoni mwetu kuna wengine wana utu wenye thamani zaidi ya utu wa wengine? Kama kuna kipimo cha utu, huo utu unapimwa na kipimo cha aina gani? Je kipimo hicho ni maumbile yetu au ni tabia zetu? ama ni vitu vinavyo tuzunguka? Muandishi anajaribu kuuliza haya maswali, kupitia muhusika mkuu wa riwaya hii ambaye ni 'SINAUBI'. Mbwana Kidato ni mtengenezaji wa vipindi vya runinga na filamu. Amepata elimu yake nchini Uingereza kwenye nyanja za uandaaji, utengenezaji, uandishi na uhariri wa picha za vipindi vya filamu na runinga. Ameshawahi kufanya kazi na Shirika la Utangazaji la Tanzania, kama mtayarishaji wa vipindi. Siyo mara yake ya kwanza kuandika, (film scripts) lakini kazi yake imekuwa ikilenga zaidi hadhara ya upande wa runinga. Safari hii ameandika riwaya/tamthilia kwa hadhara yote, yaani hadhara ya wasomaji vitabu na hadhara ya waangaliaji runinga na filamu.

  • af John W. Wanyonyi
    333,95 kr.

    Mfanisi anaanza safari yake ya kujisaka punde akiwa shuleni katika madarasa ya malezi na chekechea. Anatembea katika dunia hii ambayo anajiona akiwa pekee katika ulimwengu wa familia za wazazi wote wawili, kinyume naye aliye na mama pekee. Dunia yake inampelekea kuwa na marafiki tofautitofauti kuanzia Moi's Bridge huko Kenya, Mwanza Tanzania na mara tena Nakuru na Mombasa nchini Kenya. Maisha yake, kimsingi yanaathiriwa pakubwa na ama marafiki zake au familia yake. Katika riwaya hii utakumbana na maudhui mseto yanayoathiri kizazi cha leo na kijacho. Imeyaangazia maudhui mbalimbali kama vile maisha katika ndoa, mahusiano ya vijana kwa vijana, mahusiano ya wazee kwa vijana na wazee kwa wazee, talanta, elimu, bidii na kazi, usaliti katika maisha, unafiki, siasa na uongozi n.k. Ni kazi inayomulika maisha ya leo na jinsi masuala ibuka yanavyoathiri jamii kwa namna hasi au chanya na ni kazi ya aina yake na ambayo hutajutia kuiweka mkononi kuisoma.

  • af Lucas Lubango
    333,95 kr.

    Usiku huo nilikuwa nasimamia maandalizi ya masomo ya usiku. Nikapigiwa simu na Rose, nikaipokea. Wakati naongea naye, nikawa natembea taratibu kama naelekea kwenye mabweni. Ghafla, nikaona taa za bweni wanalolala "Buibui" zinawaka na kuzima, nikajua ni hitilafu katika mfumo wa umeme. Nikataka kusogea ili nithibitishe kisha nitoe taarifa mapema kwa uongozi na matengenezo yafanyike. Nilisogea mpaka mlangoni, taa zikawaka moja kwa moja, na kwa kuwa kulikuwa na dalili za kuwemo mwanafunzi, nilitaka kujua kwanini hayupo darasani wakati wenzake wote walikuwa wana-jisomea. Nilingia nikakuta hali ya ukimya sana, nikatembea mpaka karibu na mwisho wa bweni, nilichokiona ni aibu kubwa! Huwezi amini, "Buibui" waliponiona wakadondosha khanga! Wakabaki kama walivyozaliwa..LUCAS GERVAS LUBANGO ni mwalimu wa masomo ya biashara alivesoma Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Kibaha (ECA). Elimu ya juu aliipata katika chuo kikuu cha Dares salaam, akisomea Shahada ya Ualimu katika Masomo ya Biashara. Bweni la Wasichana ni riwaya yake ya kwanza na imeshika nafasi ya pili kwenye Tuzo ya Safal Cornel.

  • af Mohammed Khelef Ghassani
    333,95 kr.

    Tungo nyingi zilizomo humu ziliandikwa baina ya robo ya mwisho ya mwaka 2010 na nusu ya mwanzo ya mwaka 2015. Hii ni miaka mitano ya mwanzo ya mshairi kuhamia na kuishi nchini Ujerumani - mbali na nyumbani kwao, Zanzibar. Ndani yake, kwa hivyo, muna muakisiko wa hisia za mgeni ugenini, akitayamani mengi mazuri ya kwao na akijutia kuyaacha nyuma yake. Ukweli ni kuwa wakati mtu anapoishi ugenini, ndipo hasa ile thamani ya kwao anapoitambua na kutaka kuitambulisha navo zaidi na zaidi. Ndipo hisia za kutambuwa kuwa ana kwao zinapopanda kiwango cha juu. Kutoka kipembe cha mbali, Mohammed Ghassanani anakuangalia kwao na kuyaona mambo ambayo alipokuwamo ndani yake, alikuwa hata hajui kama yapo. Chembilecho Wajapani: "Samaki hajijui kuwa amerowa!" Na sababu ya kutokujijuwa huko, kwa hakika, ni kwa kuwa yeye mwenyewe anaishi ndani ya maji muda wote.¿¿¿¿¿Mohammed Ghassani alizaliwa kisiwani Pemba mwaka 1977, ambako alikulia na kusomea had alipohamia kisiwani Unguja kwa ajili ya masomo na maisha mwaka 1996 a mwaka 2010 akahamia nchini Ujerumani, ambako ndiko anakoishi na kufanya kazi

  • af Enock Maregesi
    373,95 kr.

    Hii ni riwaya ya kusisimua ya kijasusi na madawa ya kulevya inayozu-ngumzia vita kati ya Tume ya Dunia ya Umoja wa Mataifa, ya kud-hibiti madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa, 'World Drugs Enforcement Commission' (WODEC); na shirika kubwa la madawa ya kulevya la Kolonia Santita (CS-14) la Kolombia na Meksiko.Inaelezea, kwa kinagaubaga, jitihada za pamoja kati ya Tume ya Dunia, Marekani na Meksiko za kuwasaka na hatimaye kuwatia nguvuni viongozi nduli wa CS-14; na kuzuia shehena (kubwa) ya madawa ya kulevya na malighai ya nyukilia: kwenda Afrika, Asia, Amerika, Ulaya - na kung'oa mizizi ya shirika la CS-14, lote, katika nchi za Hemisifia ya Magharibi - na duniani kwa jumla.Ukisoma kitabu hiki utajiuliza, "mwandishi huyu aliwezaje kusuka riwaya inayoufanya moyo kukuenda mbio, hata kukulazimu wakati mwingine kukiweka kitabu kando ili urudishe pumzi! Ukishakianza tu, hutakiacha kabla ya kujua mwisho wa vita hi kali ya kimataifa. Na kivutio kikubwa ni kuwa kiongozi wa vita hiyo kwa upande wa Umoja wa Mataifa ni Murphy Ambilikile, Mtanzania - Willy Gamba wa Karne ya 21.Hiki ni kitabu cha kwanza cha aina yake cha kimataifa katika Tanzania. Lengo lake si tu kukata kiu ya wapenzi wa riwaya za kipelelezi na kufufua mwamko wa usomaji wa vitabu; ni kuleta, hali kadhalika, ufahamu na burudani ya kimataifa kwa wasomaji wa riwaya za kiswahili.Enock Maregesi ni gwiji wa vandishi wa riwaya za kijasusi na Kolonia Santita, imeweka kiwango kipya cha juu kitakachowaumiza vichwa waandishi wengine katika kutaka kukifkia.

  • af Christopher Bundala Budebah
    293,95 kr.

    Diwani hi ina mashairi mseto yatakayomwezesha msomaji kujitanua bila ukinzani wa uguni na usiguni, usasa na umapokeo; hivyo azingatie fani, maudhui na muktadha. Dhana zilizodokezwa ni ukoloni mamboleo, usaliti, mila potofu, ukatili, unyanyasaji wa kijinsia, haki za mtoto, UKIMWI, rushwa, kiwi ya akili, uwajibikaji na nyinginezo.Christopher Bundala Budebah alizaliwa mwaka 1956 huko Maswa, Simiyu. Ni mhitimu wa M.A Kiswahili, Stashahada ya Uzamili ya Ualimu, Shahada ya Kwanza ya Sanaa za Maonyesho na Cheti cha Sanaa za Maonyesho. Mbali na tuzo ya Mabati, mwandishi aliwahi pia kushinda tuzo ya uandishi wa kazi za fashi kwenye shindano la Jubilei ya miaka 75 ya TUKI.

  • af Idrissa Haji Abdalla
    333,95 kr.

    Sauti dhaifu ya kilio cha mwanamke ilinifikia pale nilipokuwa nimesimama karibu na vichaka vikubwa vilivyoshonana mbele yangu. "Hivi ni sauti ya binadamu kweli au ni mlio wa mnyama fulani?" Nilijiuliza swali hilo ingawa sauti ile niliyoisikia ilifanana sana na kilio cha mwanamke ambaye yuko katika maumivu makali. Hali fulani ya woga ilianza kuniingia polepole. Baada ya kuanza kupatwa na woga niliamua kumfuata bibi yangu ambaye nilimwacha akiendelea kukata kuni nyuma ya vichaka vingine vilivyokuwa kushoto kwangu.Baada ya kutembea kwa hatua zisizozidi kumi nilimwona bibi akinifuata. Hapo niliamua kusimamana kumsubiri ili nim-wulize juu ya ile sauti niliyoisikia. "Nimesikia sauti kama ya mtu ambaye alilia kwa muda mrefu na mwisho akapoteza nguvu". Bibi yangu alieleza hivyo kabla ya mimi kumweleza. "Hata mimi nilisikia ile sauti, tena inaelekea ni sauti ya mwanamke. Hivi unavyoniona ndio nimeamua kutofuata tena hizo kuni, maana nimeanza kuogopa."

  • af Mfaume Hamis Mfaume
    333,95 kr.

    Sinaye Baba ni diwani yenye mashairi ya kimapokeo yaliyobeba sauti ya kilio cha kundi la watu walio- kosa malezi kutoka kwa wazazi. Sauti hizo zilizojaa jitimai, zinaonesha ni kwa namna gani kukosa malezi kunavyoweza kuathiri jamii kwa kuifanya ipotoke zaidi. Hivyo diwani hii inamfungua macho msomaji, ili aweze kuona ni kwa namna gani malezi ni jukumu la jamii nzima.Diwani hii haijaacha kitu kwani imebeba masuala mbalimbali katika jamii, burudani, siasa na uchumi.

  • af Jane Rarieya
    448,95 kr.

    This book is a result of the Kenya National Education conference held In 2019 organised by the Aga Khan University-Institute for Educational Development, East Africa. The conference focused on contextually relevant issues affecting education in East Africa. The conference was held against the backdrop of a myriad of changes and reforms in the education sector in Kenya. These reforms have consistently not achieved the desiredoutcomes. Indeed some argue that if Kenya is to achieve Vision 2030 which aims to transform the country into a newly industrialising middle-income country providing a high quality of life to all its citizens in a clean and secure environment, education reform must be effective.

  • af Abdulrazak Gurnah
    308,95 kr.

    Swahili translation of the Nobel-prize winning author's 1994 novel Paradise.¿Mzaliwa wa Afrika ya Mashariki, Yusuf anaondoka kwao kwa ghafla akiwa na umri wa miaka kumi na mbili. Haimjii hata kwa sekunde moja, kwamba atakuwa mbali na wazazi wake kwa muda mrefu, na wala hafikirii kuuliza atarudi lini au kwa nini safari iliandaliwa kwa ghafla kiasi kile. Yusuf anaamini kuwa anamsindikiza Ami Aziz lakini ukweli ni kwamba 'ami' yake ni Mfanyabiashara, tena tajiri mkubwa, na Yusuf amewekwa rehani ili kulipia madeni ya baba yake. Yusuf anajikuta anasafiri katika miji na vitongoji vingi vingine ambako anakutana na watu wa kila namna. Anabalehe na kukua kwenye dunia inayobadilika kwa kasi kutokana na kuingia kwa ukoloni na udhalimu wake na jamii kuharibika kwa kuvurugwa kwa utamaduni wake. Hii ni tafsiri ya kwanza kwa riwaya za Abdulrazak Gurnah katika lugha ya Kiafrika.Abdulrazak Gurnah ni mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi ya mwaka 2021. Ameandika riwaya kumi ikiwemo hii ya paradise. Gurnah ni Profesa wa Masomo ya Kiingereza na Fasihi za Kikoloni katika Chuo Kikuu cha Kent.Dkt. Ida Hadjivayanis ni Mhadhiri Mwandamizi wa Masomo ya Kiswahili SOAS, Chuo kikuu cha London. Ametafsiri riwaya kadhaa kwa Kiswahili na Kiingereza.

  • af Msia Kibona Clark Kibona Clark
    492,95 kr.

    From Tamale to Paris, Hong Kong to Texas and back to Ouagadougou, this collection of scholarly chapters, poetry and personal essays theorizes the lives of African women and people of marginalized genders on the continent and the diaspora. The book is an important intervention in conversations on social movements and their convergence with digital media and other praxis tools. The contributors bring a refreshing perspective to discourses on African feminists' agency and how this manifests in their organizing in the physical world and in the digital public sphere. The volume demonstrates the relationships between the struggles of African feminists on the continent and the diaspora charting pathways for African scholars to build coalitions and work toward collective liberation.

  • af Peter Adwork Nyaba
    423,95 kr.

  • af Anna Samwel Manyanza
    243,95 kr.

  • af Samuel Andema
    748,95 kr.

  • af Shoonie Hartwig
    258,95 kr.

  • - na hadithi nyingine
    af Ally Yusufu Mugenzi
    308,95 kr.

    Hadithi hizi pia zimekuwa zikitumiwa na wakuza mitaala wa Kiswahili nchini Rwanda shuleni na zimewafurahisha wapenzi wengine wa fasihi nje ya shule.

  • af E a Musiba
    278,95 kr.

  • af Shaaban Robert
    363,95 kr.

  • af Shaaban Robert
    363,95 kr.

  • af Zainab Alwi Baharoon
    278,95 kr.

  • af Mohammed Khelef Ghassani
    278,95 kr.

  • af Ali Hilal
    278,95 kr.

Gør som tusindvis af andre bogelskere

Tilmeld dig nyhedsbrevet og få gode tilbud og inspiration til din næste læsning.